Ijumaa 13 Novemba 2026 - 10:19
Jumuiya Khoja Ithnaasharia Kampala, Yaadhimisha Siku za Fatimiyyah; Waumini Wakumbuka Mateso na Shahada ya Bibi Fatimah Zahraa (as)

Hawza/ Jumuiya ya Kiislamu ya Kishia ya Khoja Jijini Kampala Uganda, imefanya majlisi maalumu ya maombolezo kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya shahada ya Bibi Fatimah Zahraa (as), binti mtukufu wa Mtume Muhammad (saww), katika siku za maombolezo zinazojulikana kama Ayaam-e-Fatimiyyah.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Majlisi hiyo, iliyofanyika jana katika usiku uliojaa huzuni, mapenzi na kumkumbuka Bibi Fatimah Zahraa (as), iliwakutanisha waumini mbalimbali kwa lengo la kuyaenzi maisha yake matukufu, kutafakari historia ya mateso aliyoyapitia na kuhuisha mafundisho yake pamoja na mafundisho ya Ahlul-Bayt (as).

Maadhimisho hayo yalikuwa sehemu ya siku ya tatu ya Masiku ya Fa'timiyyah 1448 Hijria, kipindi ambacho wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) katika maeneo mbalimbali duniani hukusanyika katika majlisi za maombolezo ili kuonesha mapenzi na heshima zao kwa binti huyo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww).

Kwa waumini, kumbukumbu ya shahada ya Bibi Fatimah Zahraa (as) si tukio la huzuni pekee, bali pia ni fursa ya kujifunza kutoka katika maisha yake yaliyojaa imani, ibada, subira, kujitolea na kusimama imara katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Hakika, jina la Bibi Fatimah Zahraa (as) linaendelea kuishi katika nyoyo za wapenzi wa Ahlul-Bayt (as), licha ya kupita karne nyingi, mapenzi na huzuni ya kumkumbuka bado yanazidi kuunganisha waumini katika kumuenzi na kushikamana na njia ya familia tukufu ya Mtume (saww).

Jumuiya Khoja Ithnaasharia Kampala, Yaadhimisha Siku za Fatimiyyah; Waumini Wakumbuka Mateso na Shahada ya Bibi Fatimah Zahraa (as)

Jumuiya Khoja Ithnaasharia Kampala, Yaadhimisha Siku za Fatimiyyah; Waumini Wakumbuka Mateso na Shahada ya Bibi Fatimah Zahraa (as)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha